- 2,394 viewsDuration: 3:06Familia ya Eric Otieno, mhudumu wa boda boda aliyefariki katika njia tata baada ya kukamatwa na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga Jumamosi, sasa inawataka maafisa wa polisi waliotangamana naye kukamatwa. Otieno, anayedaiwa kudhulumiwa ndani ya kituo hicho cha polisi, alifariki dakika chache baada ya kuachiliwa huru huku ukaguzi wa maiti ukithibitisha kuwa alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata tumboni baada ya kupigwa vibaya.