Skip to main content
Skip to main content

Gachagua aapa kuunganisha Mlima Kenya

  • | Citizen TV
    3,235 views
    Duration: 2:53
    Kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, ameapa kuhakikisha eneo la Mlima Kenya linaelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao likizungumza kwa sauti moja, huku akionya dhidi ya juhudi za kuligawa eneo hilo kati ya Mashariki na Magharibi. Akizungumza akiwa katika ziara ya kaunti ya Meru, Gachagua aliendelea kumwonya Waziri Geoffrey Ruku dhidi ya kuendeleza mjadala wa kugawa kura za Mlima Kenya. Gachagua alidai kuwa pendekezo hilo lina msukumo wa Rais William Ruto, akisema linalenga kudhoofisha umoja wa eneo hilo kabla ya uchaguzi. Kamau Mwangi ana taarifa hiyo.