Skip to main content
Skip to main content

Gachagua adai hongo ya Sh2 bilioni katika zabuni ya Miru Systems

  • | Citizen TV
    6,705 views
    Duration: 2:51
    Kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, ameendelea kutoa madai zaidi, sasa akidai makamishna wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pamoja na Rais William Ruto walipokea hongo ya Sh2 bilioni ili kuipa kampuni ya Korea Kusini ya Miru Systems zabuni ya teknolojia ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Akizungumza alipokuwa akiondoka nchini kuelekea Marekani jana usiku, Gachagua pia alimtaka Rais Ruto kuwafuta kazi Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, na Katibu wa Usalama, Dkt. Raymond Omollo, akiwalaumu kwa kushindwa kukabiliana na wahuni nchini.