- 5,083 viewsDuration: 1:25Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anadai kuwa Rais William Ruto ana njama ya kusaini mkataba wa kuuza madini kutoka eneo la Mrima Kaunti ya Kwale kwa kampuni ya kigeni. Gachagua anadai kuwa madini kutoka Mrima tayari yanapangwa kukabidhiwa kampuni ya kigeni na kuwaacha wakazi wa eneo hilo kwenye hali ya umaskini bila kufaidi lolote. Gachagua amezungumza haya wakati wa mkutano na Wakenya wanaoishi jimbo la Kansas nchini Marekani alikodai kuwa Rais Ruto pia analenga kufaidi kwenye mkataba huo.