Skip to main content
Skip to main content

Gachagua akataa madai ya matamshi ya chuki, asema yuko tayari kujibu NCIC

  • | Citizen TV
    11,630 views
    Duration: 3:26
    Dakika chache baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa viongozi wanaochunguzwa na Tume ya Uwiano nchini, Kinara wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua amekana kutoa semi zozote za kutenganisha taifa. Akizungumza alipohitimisha ziara yake ya Kaunti ya Meru, Gachagua amesema yuko tayari kujieleza kwa tume hiyo, huku akiapa kuendelea kutumia methali na semi zinazofikisha ujumbe wake kwa eneo hilo. Na kama anavyoarifu Kamau Mwangi, Gachagua vilevile amesema alimuonya Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa angeanza kuteswa serikalini, baada ya madai kuibuka kuwa ameondolewa baadhi ya majukumu.