- 2,244 viewsDuration: 3:01Kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, amesema hatokubali eneo la Mlima Kenya kugawanywa kati ya Mashariki na Magharibi, akisisitiza kuwa umoja wa eneo hilo ndio unaolipa nguvu za kisiasa. Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kaunti ya Meru, Gachagua alisema pendekezo la kuigawa Mlima Kenya ni njama ya Rais William Ruto ya kujijengea mazingira ya kurejea mamlakani kwa muhula wa pili. Aidha, aliwahimiza wakazi wa eneo hilo kuendelea kushikamana ili kulinda maslahi yao ya kisiasa. Kamau Mwangi ana taarifa zaidi.