- 6,042 viewsDuration: 2:55Kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, amewatahadharisha wakaazi wa Mlima Kenya dhidi ya kujiunga na vyama vipya vinavyochipuka katika eneo hilo, akisema vinahatarisha kugawanya kura za eneo hilo. Akizungumza alipozuru Kaunti ya Murang’a Alhamisi, Gachagua amemtaja Rais William Ruto kuwa muasisi wa vyama hivyo vipya, akidai vinakusudiwa kugawanya kura za Mlima Kenya. Wakati huo huo, wandani wa Gachagua wamesema kinara wao hatafika mbele ya NCIC kama alivyoagizwa, wakilalamikia kile walichokitaja kuwa ni upendeleo wa tume hiyo.