- 3,659 viewsDuration: 2:53Siasa za ubabe wa Mlima Kenya zinaendelea kushika kasi huku kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, akidai kuwa Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki anatumiwa na Rais William Ruto kuwagawa wakazi wa Mlima Kenya. Akizungumza katika Kaunti ya Embu, Gachagua amesema Kindiki anajaribu kuwatumia wazee wa kijamii kuwagawa wakazi wa Mashariki na Magharibi mwa Mlima Kenya. Hata hivyo, Gachagua amesisitiza kuwa eneo hilo limeazimia kumtimua Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.