- 1,845 viewsDuration: 1:12Gavana wa Kaunti ya Murang’a, Dkt. Irungu Kang’ata, ameishutumu serikali kuu kwa kusitisha mfumo wa kidijitali wa afya wa Kaunti ya Murang’a unaojulikana kama 'Afya.KE'. Akizungumza katika Kanisa la AIPCA Cathedral mjini Nyahururu, Kang’ata alisema kuwa utawala wake umechukua zaidi ya miaka minne kujenga mfumo huo, ambao hutoa huduma za matibabu bila malipo kwa takriban boma zaidi ya 40,000 zilizo katika mazingira magumu na umaskini .