- 359 viewsDuration: 1:46Gavana wa kaunti ya Kiambu ambaye amehusishwaa naa kituo cha kibiashara ambacho kilibomolewa mapema leo hapa jijini Nairobi amekanusha kuwepo na notisi ya kumtaka ahamishe biashara yake kutoka ardhi ya shirika la reli. Kimani wamatangi amesema yeye na wafanyibiashara ambao walikodisha maduka katika kituo hicho hawakupewa ilani na walikuwa wanafanyabiashara kihalali. Wamatangi anadai tukio hilo ni la kisiasa na halihusisiani na mipango yoyote ya kutwaa ardhi ya shirika la reli kwa shughuli nyingine za maendele. Amesema hayo huku akilalama kuwa kando na biashara nyingine kuharibiwa, gari la mkewe ni miongoni mwa mali iliyoharibiwa.