Ni afueni kubwa kwa wagonjwa wa saratani, huku gharama ya dawa zinazotumika kutibu saratani ikitarajiwa kupungua kufuatia makubaliano kati ya serikali na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza dawa, Pfizer.Waziri wa Afya Aden Duale anasema makubaliano kati ya mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu - KEMSA- na kampuni hiyo yatawezesha bei ya dawa za kutibu aina saba za saratani kupungua zaidi ya mara saba. Aidha Duale anasema kuwa hali hiyo itawezesha SHA kugharamia kikamilifu matibabu ya saratani kwa shilingi laki nane zilizotengewa matibabu hayo. Mary Muoki anaarifu zaidi.