- 456 viewsDuration: 3:16Hofu ya uhaba wa chakula inaendelea kuongezeka katika Kaunti ya Baringo baada ya mazao kuharibika kutokana na ukame, kuongezeka kwa viwango vya maji katika maziwa ya eneo hilo na changamoto za kiusalama. Miezi kadhaa ya ukosefu wa mvua imekausha maelfu ya ekari za mashamba ya mahindi katika maeneo ya Mochongoi na Marigat. Wakulima waliokopa fedha kwa ajili ya msimu huu wa upanzi sasa wanakadiria kupata hasara badala ya mavuno. Brenda Wanga anatuarifu zaidi.