- 919 viewsDuration: 3:16Hofu imetanda katika kijiji cha Ogago kilichoko Bondo, Kaunti ya Siaya, baada ya watu watatu kukwama ndani ya mgodi wa dhahabu. Kulingana na wakazi, watu hao walifukiwa na vifusi vya mgodi walipokuwa wakichimba dhahabu usiku wa kuamkia Jumamosi. Haya yanajiri huku familia kadhaa zikiendelea na mazishi ya watu 15 waliofariki katika mkasa wa mgodi wa Romus, Kaunti ya West Pokot.