Skip to main content
Skip to main content

Huduma za matibabu zatatizwa hospitalini Transmara mjini Kilgoris

  • | Citizen TV
    116 views
    Duration: 1:37
    Huduma za matibabu katika hospitali ya Trannsmara West mjini Kilgoris zimetatizika pakubwa baada ya usimamizi wa hospitali hiyo kuamua kuifunga ghafla kufuatia tukio la uvamizi wa wahudumu wa afya usiku wa kuamkia jumatano na kuacha maafisa wa afya na majeraha. Kwa mujibu wa baadhi ya maafisa katika hospitali hiyo ambao hawakutaka kutajwa, wahuni waliojihami walifika ndani ya hospitali ya Transmara West usiku huo wakiwa na mgonjwa aliyehusika katika ajali na kuzua vurugu baada ya mgonjwa wao kushauriwa kupata matibabu katika hospitali moja ya misheni kufuatia hali yake mbaya , kilochofuata ni manesi kupigwa na kuachwa na majeraha mabaya mwilini.