Skip to main content
Skip to main content

IEBC yamtoza mbunge wa Kipiri Wanjiku Muhia faini ya Sh1.5 milioni kwa kutoa matamshi ya uchochezi

  • | Citizen TV
    7,220 views
    Duration: 2:55
    Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Independent Electoral and Boundaries Commission, imemtoza faini ya shilingi milioni moja na nusu Mbunge wa Kipipiri, Wanjiku Muhia, kwa kile inachosema ni kutoa matamshi ya chuki na uchochezi wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou. Tume hiyo imemtaka mbunge huyo kulipa faini hiyo ndani ya saa 72 na kuomba msamaha kwa umma. Aidha, IEBC imemtaka Mbunge wa Nakuru Town East, David Gikaria, kufika mbele yake kufuatia matamshi aliyotoa wiki iliyopita huko Ol Kalou.