- 6,699 viewsDuration: 3:15Jioni ya leo maafisa wa usalama wako tena kwenye darubini kwa madai ya kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa Multimedia University of Kenya hapa Nairobi. Independent Policing Oversight Authority sasa inasema inachunguza matukio haya ya mapema juma hili, ambapo wanafunzi wawili walipigwa risasi na kuachwa na majeraha ya risasi mwilini. Na kama anavyoarifu Ode Francis, maafisa waliohusika wamenaswa wazi kwenye kamera za CCTV.