Skip to main content
Skip to main content

Kalonzo ataka mageuzi, ahimiza kukamilishwa kwa barabara ya Thika–Garissa

  • | Citizen TV
    315 views
    Duration: 1:04
    Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, amesema Kenya inahitaji mageuzi makubwa, akisisitiza kuwa maendeleo ni haki ya kikatiba ya Wakenya na si hisani ya serikali. Akizungumza Tseikuru, Kaunti ya Kitui, Kalonzo alimtaka Rais William Ruto kuharakisha ujenzi wa barabara ya Thika kuelekea Garissa, akisema mradi huo umekwama kwa zaidi ya muongo mmoja. Kiongozi huyo pia aliwapongeza vijana wa Gen Z kwa kusimama kidete kutetea haki zao na kuhimiza uwajibikaji katika uongozi wa nchi. Alisema ni kupitia mageuzi, maendeleo na uongozi wenye uwajibikaji ndipo wananchi watanufaika kikamilifu na rasilimali za taifa.