Skip to main content
Skip to main content

Kaunti ya Kilifi yatenga Ksh.150m za ufadhili wa elimu

  • | Citizen TV
    175 views
    Duration: 1:23
    Huku usajili wa wanafunzi wa gredi ya 10 ukiendelea kote nchini, serikali ya kaunti ya Kilifi imetenga shilingi milioni 150 ili kusaidia wanafunzi kuendeleza masomo yao. Akizungumza na wanahabari katika ofisi yake Waziri wa elimu kaunti ya Kilifi Felkin Kaingu amesema kuwa fedha hizo zitafadhili masomo ya wale wanafunzi waliopata alama za shule za kitaifa kando na wale wanaotoka katika familia zisizojiweza. Haya yanajiri baada ya kuripotiwa visa vingi vya wazazi walioshindwa kuwapeleka Watoto wao katika shule walizopata kutokana na changamoto za kifedha .