Skip to main content
Skip to main content

Kenya kuzindua kituo cha kitaifa cha ambulansi

  • | Citizen TV
    733 views
    Duration: 3:15
    Kenya inatarajia kuzindua rasmi wiki ijayo Kituo cha Kitaifa cha Kusimamia Magari ya Kubeba Wagonjwa, hatua inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma za afya za dharura nchini. Kulingana na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), uzinduzi huo utawezesha utekelezaji kamili wa Hazina ya Huduma za Dharura yenye thamani ya shilingi bilioni sita, ambayo haijatumika kikamilifu. Aidha, wananchi wanaohitaji huduma za ambulansi watatakiwa kupiga nambari 922 ili kupata huduma za dharura kwa haraka.