Skip to main content
Skip to main content

Kenya Kwanza yapuuza mikutano ya Linda Mwananchi

  • | Citizen TV
    3,211 views
    Duration: 2:24
    Viongozi wa Kenya Kwanza wamepuuza mikutano ya mrengo wa Linda Mwananchi, wakisema haileti tishio lolote kwa muungano huo licha ya kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi. Wakizungumza katika eneo la Kitutu Chache Kaskazini, Kaunti ya Kisii, viongozi hao walidai kuwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta anahusika na kuandaliwa kwa mikutano hiyo, wakidai pia kuwa inalenga kuwapotosha wanasiasa wachanga nchini. Viongozi hao pia walimtaka Naibu Kiongozi wa Chama cha Jubilee, Fred Matiang'i, pamoja na kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, kujiunga na serikali, wakisema kuendelea kubaki upinzani kutawaathiri kisiasa. Chrispine Otieno ana taarifa zaidi.