Skip to main content
Skip to main content

Kiambu yajenga barabara licha ya kuchelewa kwa fedha

  • | Citizen TV
    5,185 views
    Duration: 3:30
    Huku kaunti mbalimbali nchini zikiendelea kukabiliwa na kucheleweshwa kwa fedha za Hazina ya Barabara kutoka kwa Serikali Kuu, Kaunti ya Kiambu imechukua mkondo tofauti kuhakikisha ajenda yake ya maendeleo inaendelea. Serikali ya Kaunti ya Kiambu imepeleka mitambo yake ya ujenzi katika mradi unaofadhiliwa na fedha za kaunti kwa lengo la kujenga na kukarabati barabara katika maeneo mbalimbali. Mpango huu tayari umeanza kubadili usafiri na kuimarisha barabara katika kaunti hiyo.