- 4,808 viewsDuration: 2:55Tukisalia kwenye siasa za mlimani, Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki naye sasa amempa ilani mtangulizi wake Rigathi Gachagua akisema kuwa siku zake za ushawishi wa Kisiasa ni za kuhesabu. Akizungumza kwenye mkutano wa wakazi wa kaunti za mashariki mw amlima kenya huko Meru, Kindiki amemtaka Gachagua na viongozi wenzake wa upinzani kuonyesha waliyowafanyia wananchi walipokuwa serikalini badala ya kuendeleza siasa za matusi. Aidha amewataka wazee wa mashariki mwa mlima kenya kutafuta uwiano na wenzao wa magharibi ili kumuunga mkono rais william ruto kwenye azma yake ya kutafuta muhula wa pili.