- 1,769 viewsDuration: 1:09Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki amemtahadharisha kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, dhidi ya kupinga kauli ya wazee wa Mlima Kenya, waliomtawaza kama msemaji wa eneo hilo. Akizungumza alipokagua miradi katika maeneo bunge ya Tharaka na Buuri, kaunti za Tharaka Nithi na Meru, Kindiki amemtaka mtangulizi wake kuheshimu maamuzi ya wazee, akisema wana jukumu la kipekee la kutoa mwelekeo kwa jamii hiyo. Kindiki amesema atatumia nafasi aliyopewa kuendeleza juhudi za kuunganisha jamii za Mlima Kenya na kuhakikisha wakazi wanashirikiana, kuelekea uchaguzi mkuu. Kauli hiyo inajiri huku mjadala kuhusu uongozi na uwakilishi wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya ukiendelea.