- 582 viewsDuration: 1:28Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki ameelezea imani kuwa serikali itashinda vita vipya dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya nchini kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza alipozuru eneo bunge la Mukurwe-ini kaunti ya Nyeri, Kindiki amesisitiza kuwa hakuna atakayesazwa kwenye vita hivyo vilivyotiwa nguvu mpya, akitishia kufungwa kwa biashara zinazoshiriki utengezaji pombe yenye maafa.