- 5,053 viewsDuration: 1:59Naibu Rais Kithure Kindiki amesema mchakato wa ujenzi wa bomba la kusafisha mafuta katika Kaunti ya Lamu umeshika kasi, huku mjadala wa kubaini upatikanaji wa ardhi kutakapojengwa bomba hilo ukiendelea. Katika kikao na mawaziri, makatibu na wakuu wa idara zilizohusika na ujenzi huo, Kindiki alirai mataifa jirani katika ukanda wa Afrika Mashariki kushirikiana na kuafikiana na mwekezaji Aliko Dangote, ili ujenzi wa bomba hilo ung'oe nanga na kukamilika kwa muda mfupi. Mradi huo unatarajiwa kufungua nafasi za ajira kwa vijana, kukuza uchumi na kutoa suluhu ya changamoto zinazoathiri bei, upatikanaji na usafirishaji wa mafuta.