Hebu tafakari haya. Serikali hutoa shilingi elfu moja mia nne na ishirini kila mwaka kufadhili masomo ya kila mwanafunzi wa shule ya msingi ya umma nchini. Katika muhula huu, Wizara ya elimu imetoa shilingi mia moja themanini na nane pekee kwa kila mwanafunzi, ambapo shilingi mbili pekee zimetengewa kugharamia masomo ya sayansi na teknolojia.Hali hiyo imesababisha Muungano wa walimu nchini KNUT kutaka majadiliano kati ya wadau katika sekta ya elimu ili kuzungumzia uhaba wa fedha katika shule za msingi. Wataalamu wa elimu wamesema kuwa uhaba huo wa fedha utaathiri mtaala wa CBE haswa katika shule za umma ambazo hutegemea fedha kutoka kwa serikali.