Skip to main content
Skip to main content

LSK yataka uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mawakili wawili

  • | Citizen TV
    1,002 views
    Duration: 2:32
    Chama cha Wanasheria nchini, LSK, kimeshutumu vikali mauaji ya mawakili Esther Wairimu Keige na Edward Muthee Kariuki, ambao vifo vyao vimetokea katika mazingira yanayotajwa kuwa ya kutatanisha. Rais wa LSK, Charles Kanjama, amesema mauaji hayo ni shambulio dhidi ya utawala wa sheria na haki, na ametaka uchunguzi wa kina kufanyika, ikiwemo kupitia faili za kesi ambazo mawakili hao walikuwa wakizishughulikia. Kanjama pia ametaka kuchunguzwa kwa kesi aliyokuwa akiisimamia Wakili Keige kuhusu Idara ya Huduma za Misitu (KFS) ili kubaini iwapo kifo chake kilihusiana na utekelezaji wa majukumu yake. Na kama anavyoarifu Mary Muoki, LSK pia inataka mawakili ambao kazi zao zinawaweka katika hatari na vitisho kupewa ulinzi.