- 2,996 viewsDuration: 5:26Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini kwa kongamano la Afrika Forward Summit litakaloandaliwa nchini Jumatatu na Jumanne. Rais Macron alipokewa na mwenyeji wake Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi kabla ya kufanya mkutano wa faragha. Marais wa mataifa 30 barani Afrika wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo huku marais kumi wakiwa tayari wamewasili nchini. Kongamano hilo linalenga kusisimua biashara katika sekta za kawi, miundombinu, uchukuzi na teknolojia pamoja na sekta nyingine barani Afrika.