Skip to main content
Skip to main content

Maduro ni nani na kwanini Marekani imemkamata?

  • | BBC Swahili
    83,801 views
    Duration: 2:41
    Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, na mkewe, Cilia Flores, wamekamatwa na Marekani baada ya shambulio kubwa la kijeshi nchini humo, kulingana na taarifa za Rais wa Marekani, Donald Trump. Trump amesema kuwa operesheni hii ilifanywa kwa ushirikiano na vyombo vya sheria vya Marekani na kwamba Maduro na mke wake wamehamishwa nje ya nchi. Mlipuko uliripotiwa katika maeneo mbalimbali ya Caracas asubuhi ya Jumamosi, ikiwemo kambi za kijeshi kama La Carlota na Fuerte Tiuna. Sehemu kadhaa jirani hazina umeme, huku taarifa zisizo rasmi zikisema ndege zilikuwa zikiruka juu ya jiji. Hadi sasa, idadi ya waliopoteza maisha au kujeruhiwa haijajulikana Lakini Je, Maduro ni nani na kwanini Marekani imemkamata? @mrs.tadicha na taarifa hii: - - #bbcswahili #venezuela #trump #maduro #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw