- 1,743 viewsDuration: 2:26Mahakama ya Mombasa imembandua ofisini aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi wa bandari ya Mombasa Simon Sang kwa madai ya utumizi mbaya wa mamlaka na ukiukaji wa sheria za afisi hiyo. Kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa na baadhi ya viongozi wa muungano huo Jaji Monica Mbaru wa mahakama katika uamuzi wake amesema kwamba Uongozi wa Sang ulikwenda kinyume na katiba ya mungano huo na hivyo hakustahili kushikilia wadhifa huo. Mahakama hio pia imemuru viongozi wa muungano huo waliobanduliwa mamlakani kurudi ofisini, huku nafasi ya sang sasa ikishikiliwa na Sulman Otieno kama kaimu katibu mkuu.