Skip to main content
Skip to main content

Mahakama yasitisha kukamatwa kwa washukiwa wa Manzil Towers

  • | Citizen TV
    1,300 views
    Duration: 53s
    Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa watu watatu kuhusiana na kuporomoka kwa jengo la Manzil Towers C katika mtaa wa South C, Nairobi, hadi maombi yao yatakaposikilizwa. Katika uamuzi wake, Jaji Nabil Mokaya alimpa aliyekuwa Afisa Mkuu wa Mipango ya Miji katika Kaunti ya Nairobi, Patrick Analo, pamoja na David Kibui na John Gombe, ruhusa ya kupinga uamuzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wa kuwafungulia mashtaka kwa madai ya matumizi mabaya ya afisi kuhusiana na mkasa huo. Mahakama pia iliizuia DCI na maafisa wake kuwakamata, kuwafungulia mashtaka au kuendelea na kesi yoyote dhidi yao hadi ombi hilo litakaposikilizwa. Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 16 mwaka huu kwa maelekezo zaidi.