- 2,896 viewsDuration: 2:48Mahakama Kuu imewaamuru Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang'ula, na Spika wa Seneti, Amason Kingi, kukoma kutumia ofisi zao kupigia debe mrengo wowote wa kisiasa. Amri hiyo inafuatia ombi lililowasilishwa mahakamani likitaka maspika hao wazuiwe kutumia nyadhifa zao kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kutafuta muhula wa pili. Mahakama imesisitiza kuwa viongozi wanaoshikilia nyadhifa za umma wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kutokuwa na upendeleo wa kisiasa. Ben Kirui ana taarifa zaidi.