- 3,921 viewsDuration: 2:06Rwanda inaendelea kuboresha upatikanaji wa umeme kwa kutumia nishati ya jua, kama nguzo muhimu ya maendeleo endelevu. Kwa sasa, kuna kampeni ya kitaifa inayoendelea ya kusambaza vifaa vya umeme wa sola kwa familia zinazoishi katika maeneo ya vijijini na yaliyo mbali na miundombinu ya umeme. Kupitia ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi chini ya uratibu wa Rwanda Energy Group (REG), juhudi zinafanyika kuhakikisha kila kaya inapata huduma ya umeme. Mpango huu unatekelezwa kwa kutumia mifumo ya umeme wa gridi ya taifa (on-grid) pamoja na suluhisho mbadala za nje ya gridi (off-grid), ili kufikia hata maeneo yasiyofikika kirahisi. @yvebuchana na taarifa hii - - #bbcswahili #rwanda #solar #umeme Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw