- 4,016 viewsDuration: 3:39Risala za rambirambi na sifa zilimiminika kwa aliyekuwa Mbunge wa Lugari, Cyrus Jirongo, huku familia, marafiki na viongozi wa kisiasa wakihudhuria ibada ya wafu . Wakizungumza wakati wa ibada hiyo iliyofanyika kwa heshima yake katika Kanisa la CITAM jijini Nairobi, waombolezaji walimkumbuka Jirongo kama mtu mkarimu aliyeishi maisha kikamilifu. Hata hivyo, maswali yaliendelea kuibuka kuhusu mazingira ya kifo chake kama anavyoarifu ripota wetu Ben Kirui