- 876 viewsDuration: 2:49Waziri wa Hazina John Mbadi ameshutumu upinzani kwa kuwapotosha Wakenya kuhusu yaliyomo kwenye mswada wa fedha wa mwaka 2026. Mbadi amesisitiza kuwa mswada huo unalenga kupunguza gharama ya maisha kwa wananchi, akisema hauna mapendekezo yoyote mapya ya ushuru kama inavyodaiwa na upande wa upinzani. Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya ushuru wanasema kuwa kuna baadhi ya mapendekezo ndani ya mswada huo ambayo huenda yakamweka mwananchi katika mzigo zaidi wa kifedha.