- 401 viewsDuration: 59sMbunge wa Likuyani Innocent Mugabe amerai wakazi wa eneo la Magharibi mwa Kenya kumpigia kura tena Rais William Ruto kwenye uchaguzi ujao kutokana na utndakazi wake. Akizungumza alipokuwa mwenyeji wa rais William Ruto kwenye ibada katika kanisa katoliki la Marko Matunda eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega, kiongozi, Mugabe alisema kwamba tayari miradi mbali mbali kama vile barabara zinaendelea kujengwa kwa lengo la kuboresha uchukuzi na kilimo katika eneo la Magharibi.