- 1,601 viewsDuration: 3:12Tunaanza taarifa zetu na mgomo wa wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu ulioingia wiki ya pili, huku wanafunzi wakiendelea kukosa masomo mgomo huo unapoendelea. Walimu wakiendelea kusisitiza kuwa hawatarejea darasani hadi serikali itekeleze matakwa yao, wanafunzi sasa wanaitaka serikali na wahadhiri kufikia mwafaka haraka ili kuhakikisha masomo yao yanaendelea. Katika baadhi ya vyuo vikuu tulivyozuru leo, wanafunzi wanasema wanaendelea kugharamika kutokana na mgomo huo.