- 23,152 viewsDuration: 2:45Maafisa wa usalama wamefanikiwa kupata miili na mabaki ya watu saba walioangamia katika ajali ya ndege iliyotokea katika Mlima Ololokwe, Kaunti ya Samburu. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Samburu, David Nkoroi, amesema shughuli za uokoaji zimekamilika na miili yote imesafirishwa hadi katika Mochari ya Lee hapa Nairobi, kwa ajili ya uchunguzi wa maiti utakaofanyika kesho. Imebainika kuwa miongoni mwa waliofariki ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujasusi wa Ecuador.