Skip to main content
Skip to main content

Motsepe aridhishwa na maandalizi ya Kenya kwa AFCON 2027

  • | Citizen TV
    1,931 views
    Duration: 47s
    Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe, ameeleza kuridhishwa na maandalizi ya Kenya kuelekea michuano ya AFCON 2027. Akizungumza baada ya kufanya ziara katika viwanja vya Kasarani na Talanta hapa jijini Nairobi, Motsepe amesema ana imani kuwa kufikia mwezi Disemba, kazi zilizosalia zitakuwa zimekamilika katika viwanja hivyo. Ameahidi kurejea nchini mwezi Januari ili kuhakikisha kila kitu kiko tayari kwa dimba la AFCON litakaloandaliwa mwezi Juni na Julai 2027 kwa ushirikiano wa Kenya, Tanzania na Uganda. Kuhusu nchi zitakazoandaa mechi za ufunguzi na fainali, Motsepe amesema majadiliano yanaendelea.