Skip to main content
Skip to main content

Mpango wa visima 27 vya nishati ya jua wapa matumaini wakazi wa Kwale

  • | Citizen TV
    435 views
    Duration: 3:06
    Kwa miaka mingi, wakazi wa baadhi ya maeneo ya Kwale wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kutafuta maji, huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa wa kutafuta bidhaa hiyo muhimu. Lakini sasa, matumaini mapya yameanza kuchomoza baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa kuweka mtambo wa kupiga maji wa nishati ya jua katika visima vya maji 27 katika maeneo tofauti .