- 4,077 viewsDuration: 3:02Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amemtetea Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki, akisema ndiye atakayekuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Mudavadi anasisitiza kuwa Kindiki ni kiongozi mwaminifu aliyeleta heshima kwa serikali ya Rais Ruto na hivyo atasalia kuwa naibu wake, licha ya shinikizo kutoka kwa washirika wa serikali katika serikali jumuishi wanaotaka nafasi hiyo. Hayo yanajiri huku Kindiki akisifia utendakazi wa Rais William Ruto katika miaka minne ya utawala wake.