- 1,978 viewsDuration: 1:35Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema hana nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao na badala yake atamuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kutafuta muhula wa pili. Akizungumza katika kaunti ya Trans Nzoia, Mudavadi amesema analenga kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2032. Wakati huo huo, viongozi wa Kenya Kwanza waliokutana kaunti ya Kericho wameitaka Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, NCIC, pamoja na Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa madai ya uchochezi.