Skip to main content
Skip to main content

Muuaji wa familia ahukumiwa kifo mara nne

  • | Citizen TV
    9,599 views
    Duration: 2:21
    Mahakama Kuu ya Kisumu imemhukumu mwanamume mmoja adhabu ya kifo mara nne baada ya kukiri mashtaka ya mauaji. Shem Akuku, mwenye umri wa miaka 30, aliwaua jamaa zake wanne kwa kuwashambulia kwa panga, wakiwemo mkewe na mwanawe wa miaka saba. Mahakama ilisema uzito wa makosa aliyopatikana nayo na mazingira ya uhalifu huo yanawiana na adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria za Kenya. Laura Otieno ana taarifa hiyo.