- 4,122 viewsDuration: 7:00Waathiriwa wa mapigano ya Ang'ata Barrikoi wakiendelea kuwa kambini baada ya kutoroka kwao, maafisa wa upelelezi wa jinai wanasema kuwa wanashuku kuwa watu watano waliokamatwa wiki hii wanahusika na kupanga na kufadhili mapigano hayo. Haya ni huku kafyu iliyowekwa na idara ya usalama ikiendelea licha ya sikukuu. Chrispine Otieno amekuwa akifuatilia kwa karibu machafuko katika eneo hilo, na sasa anatujengea taswira ya mambo yalivyokuwa na yalivyo katika kaunti za Kisii na Narok.