- 8,795 viewsDuration: 4:39Maziara ya Kang’o ka Jaramogi alikozikwa Raila Amolo Odinga huko Bondo yanaendelea kushuhudia msisimko, ngoma, densi na maombi kila siku, wiki kumi baada ya mazishi yake. Maelfu ya waombolezaji na wanaofika hapo kutoa heshima zao wamekuwa wakitumbuizwa na ngoma na nyimbo za kundi moja la kitamaduni ambalo limekuwa hapo siku zote. TMatukio hayo pia yamefufua biashara za wakazi wa eneo hilo ambalo kawaida huwa halina shughuli nyingi. Brenda Wanga na taswira kamili.