Mwanamke Bomba: Kwa takriban miaka sita sasa, Caroline Njeri Ng'ang'a amekuwa tegemeo la baadhi ya watu kiuchumi, si hapa jijini Nairobi pekee, bali pia kwa kina mama kutoka Turkana, Kitui na Makueni. Biashara ambayo aliianza kama njia ya kusaidia kina mama kupata soko la bidhaa zao nje ya nchi sasa imekuwa uti wa mgongo kwa zaidi ya familia 50 kupitia ajira.
Caroline, ambaye ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Crafts With Meaning, anatueleza mengi kuhusu safari yake na namna anavyojiimarisha licha ya changamoto za hapa na pale.