Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ameishauri Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kuwa makini katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Mwilu amesema ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 zinapaswa kuwa funzo kwa Wakenya na kwa IEBC kuhusu umuhimu wa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru, haki na unaoaminika.
Akizungumza katika kikao kilichoandaliwa na IEBC jijini Nairobi, tume hiyo imeahidi kuendesha uchaguzi mkuu ujao kwa njia ya huru, haki na yenye uwazi.
Seth Olale anaripoti.