- 2,832 viewsDuration: 3:33Kinara wa DCP Rigathi Gachagua, mawaziri Aden Duale na Geoffrey Ruku ni miongoni mwa watu 10 wanaochunguzwa na Tume ya Uwiano na Maridhiano - NCIC - kuhusiana na matamshi ambayo yanakisiwa kuwa ya chuki. Tume hiyo inasema imeanzisha uchunguzi kufuatia malalamishi kutoka kwa Wakenya. Gavana wa Busia Paul Otuoma, naibu gavana wa Mandera Ali Maalim Mohamud, na wabunge watatu pia wanachunguzwa. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, tume hiyo inasisitiza kuwa itachunguza madai yote bila upendeleo.