- 16,775 viewsDuration: 2:43Tume ya Uwiano na Utangamano nchini (NCIC) imemtaka kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, kufika mbele yake Alhamisi wiki ijayo. NCIC imesema inachunguza matamshi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi yaliyotolewa na Gachagua katika mikutano tofauti ya kisiasa. Aidha, NCIC imemtaka Gavana wa Busia, Paul Otuoma, kufika mbele yake, huku Chama cha Mawakili nchini (LSK) kikichunguza pia matamshi ya Mbunge wa Mukurweini, John Kaguchia, na Peter Kaluma wa Homa Bay.