- 2,978 viewsDuration: 1:11Kinara wa chama cha Peoples Party of Kenya, Ndindi Nyoro, sasa anadai kwamba viongozi wakuu serikalini ndio walipanga kuilaghai serikali ya Uganda kwenye mkataba wa mafuta. Nyoro anasema mpango huo ulifanywa kwa kupandisha bei ya mafuta, huku wahusika wakijinufaisha wenyewe. Akiongoza mkutano wa kisiasa katika eneo la Njiru, eneo bunge la Kasarani, mbunge huyo wa Kiharu pia amemtaka Rais William Ruto kukoma kumzungumzia Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.